God’s Time | Wakati wa Mungu

Chochote unachotamani kuwa nacho katika maisha haya tuliyonayo hapa duniani yamefungwa katika muda hakuna kitu ambacho kipo tu tayari wakati wote. Vyote vipo lakina vitapita kupisha majira ya kingine kuja. Katika chochote unachotamani kukipata lazima ujiulize ni wakati sahihi wa mimi kuwa nacho? Au nina stahili hiki kuwa nacho? na kwanini sina kwa wakati huu?

Mhubiri 3:1-11

Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa; Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka....

Sasa ni nini kinafanya tusiweze kuona fursa iliyopo katika majira?? Moja ya sababu inayopelekea kutokuona fursa katika majira uliyopo:- Kutokujua namna ya kumwabudu Mungu katika Roho!
Watu wengi na wakristo wengi ukiwaambia kwa habari ya kuabudu anafikiri na kuelewa ni kwenda kanisani siku ya Jumapili, kuimba nyimbo na wanakwaya au waongoza sifa na maabudu wakiongoza huko ndiko kuabudu. Lakini ni nini maana halisi ya kuabudu?

Kuabudu ni tendo la kumpa Mungu heshima ya juu, utukufu, na utii wa dhati kutoka moyoni, linaloambatana na kusujudu, kusifu, na kujitoa kikamilifu. Hii si taratibu tu ya kidini, bali ni uhusiano binafsi, utambuzi wa ukuu wake, na maisha ya kumthamini Mungu kuliko kitu chochote.

Na neema ya Mungu ikiwa juu ya mtu katika majira sahihi juu ya huyo mtu, atakula mema au wema wa Mungu. Mungu huwa anafanya majira katika pande mbili kwenye maisha ya mtu, upande wa mazuri na upande wa mabaya. Pande zote mbili za majira haya lazima zitokee juu yako. Kazi yako wewe ni kukubaliana na hayo majira ukiwa na hakika kuwa ninapitia kipindi kigumu lakini ni Mungu ameamuru haya, hivyo ukikubali unampa Mungu nafasi ya kuingilia kati hilo jambo/hitaji lako.

Mfano mzuri tulio nao ni wa Yesu mwenyewe! Kama Yesu asingekubaliana na majira mabaya ya kusalitiwa na Yuda tusingekuwa na neema ya wokovu tulio nao sasa. Majira yanapokuja unatakiwa kukubaliana nayo nakumruhusu Mungu kutimiza mapenzi yake juu yako. (Lay down your will for his will!)

Kuna namna baadhi ya wakristo wanaamini ni wakati wa mazuri tu, ndio wakati sahihi wa Mungu. Hapana! Uwelewa huu sio sahihi. Kwani Mungu anaweza kukupitisha katika majira ya furaha, majonzi na majira ya kusubiri. Na katika majira ya majonzi au kusubiri sio kwa sababu umemkosea au haustahili! Ni wakati wa yeye kukunoa, kukupitisha katika mafunzo kwa habari ya kile anachokikusudia kwako. Ni kipindi cha maandalizi.

Mfano mwingine katika maandiko ni Elizabeth na Zakaria. Walikua ni wenye haki mbele za Bwana lakini hata katika umri wao hawakua wamebarikiwa na mtoto bado. Tukisoma Luka 1:5-8 tunaona hii habari.

Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti.Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana.Basi ikawa, alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu,

Kwanini Mungu ameweka majira katika maisha yetu?

1.Ili tujifunze kumwamini, kumwabudu yeye na kumtegemea yeye katika nyakati na hali zote.

Kuamini ni nini? Uamini ni kitendo cha kuwa na hakika, utii, ushawishi, au tumaini thabiti juu ya jambo, mtu, au Mungu, hata bila kuona uthibitisho katika macho ya nyama.
Mungu hapendi umwabudu yeye halafu unategemea na msaada kwingine, iwe vitu au watu. Anachotaka umwangalie yeye tu!

Zaburi 125:1

Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni,Ambao hautatikisika, wakaa milele.

    2.Kututengenezea Msuri wa kumtukuza, kumshukuru na kumrudishia yeye utukufu katika kile alicho au anachotegemea kukubariki nacho.

    3.Ni kuruhusu yeye akupeleke pahala sahihi.

    2 thoughts on “God’s Time | Wakati wa Mungu”

    Leave a Comment

    Your email address will not be published. Required fields are marked *