Uzuri wa kushikwa mkono na Mungu.

Kuna mikono mingi sana inatamani itushike wakati tunapita wakati flani au katika safari flani kwenye maisha. Inaweza kua na nia iliyo nzuri na pia inaweza isiwe na nia nzuri pia katika kukushika mkono. Ila, Mungu akikushika mkono, ni ishara yuko na wewe. Ni kiongozi wa maisha yako, ni ishara ya ulinzi wa Mungu juu yako na maisha yako na msaada wake kwako! Katika kila hatua atahakikisha anakushika kwa mkono wake wa kuume!

Ni muhimu sana kuweka sahihi katika maombi yako. Kuweka sahihi kwa mantiki kua umemkabidhi Mungu. Umetia mhuri kua hili nakuachia wewe Mungu ,ni lako kulitatua na yeye ndio atatenda. Umemuamini na imani yako ni asilimia mia moja kwake katika kila jambo. Na hio ni moja ya mlango wa Mungu kukushika mkono kikamilifu kwa maana umeachilia vyote kwake.

Kuna uzuri mkubwa sana wa kushikwa mkono na Mungu kwa sababu kiwango atakushika hakuna binadamu yeyote angeweza kukupitisha! Inafika sehemu huna la kujieleza juu ya umewezaje au ilikuwaje! Kwa maana haufahamu mkono wake ulikubeba au kukushika kwa namna gani.

Faida za kushikwa mkono na Mungu.

1.Mungu akikushika mkono una uhakika wa usalama na ulinzi katika maisha yako.

    Isaya 41:13

    'Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia. '

    Akikushika atakuambia habari juu ya maisha yako, juu ya kila uwalakini utaokua nao kwenye jambo lolote, hatanyamaza atakuongoza. Hii inakupa uhakika ni wapi utakua salama na ulinzi wake ukiwa umeshikwa mkono na Mungu. Pamoja na magumu unayoweza kupitia katika maisha, hata katika maumivu tunayoyasikia bado tusiwe kama wengne, ambao hawana uhakika wa Yesu waliye nae! Kwa maana amesema usiogope ntakusaidia! Hautakua peke yako katika kila hatua utayosogea, atatembea na wewe atakua na wewe kila hatua uendayo.

    Hii ina maana kua mfahamu sana Mungu na uwe na uhusiano naye wewe binafsi. Uhusiano wa kiwango cha kuamini neno la Isaya 41:13. Kwa namna hiyo ni rahisi kuwa na uhakika Mungu amekushika mkono.

    2. Mungu akikushika mkono unakua na uongozi sahihi.

    Zaburi 37:23-24

    Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA, Naye aipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, BWANA humshika mkono na kumtegemeza.

    Unapata mwelekeo sahihi katika kila jambo lako. Tunafahamu, kadri unavyopambana kuenda mbele shetani nae anatamani usisonge mbele, ujikwae! Hivyo Mungu akikushika mkono hatua zako zitaimarishwa nae na atakutegemeza. Katika majira hayo Mungu anakua yeye mwenyewe anakutegemeza kwasababu amekushika mkono!

    Katika Mithali 16:9 neno la Mungu linasema, "Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake."

    Hata pale adui anapotaka urudi nyuma, kwa mkono wa Mungu aliokushika hautarudi nyuma, maana hatua zako anaziimarisha Mungu kwa mkono wake wa kuume. Kila unachokifanya kinakua kinaenda kwa namna ya kibali cha kipee kwa sababu hatua zako ni yeye anaziongoza!

    3. Mungu akikushika mkono Hofu inaondoka moyoni mwako.

    Kumb 31:8

    Naye BWANA, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.

    Kuna wakati tunaomba tunahisi Mungu hajibu ila anajibu. Na kuna wakati unahisi yupo kimya na unaanza kua na hofu, mbona hakuna njia, mbona hakuna pa kutokea, lakini ukiwa na uhakika Mungu amekushika mkono hutaogopa mana amesema hatakupungukia wala kukuacha na wala usiogope. Ukiona hofu inaingia, imani yako imeshuka na kuamini kwako kwamba Mungu kakushika mkono kumeshuka. Hivyo hima imarisha imani yako mana amesema hakika hatokuacha na neno lake ni hakika!

    Mungu ameshachagua kukushika mkono na kukaa na wewe ni milele atakua na wewe ina maana ni wewe kuishi hio ahadi na hilo neno alilolisema mana kamwe hatopungua kwako!

    1 thought on “Uzuri wa kushikwa mkono na Mungu.”

    Leave a Comment

    Your email address will not be published. Required fields are marked *